DEREVA DARAJA II (DRIVER II)
Employer: Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Salary Scale: TGS B
Posts: 22
Closing Date: 06 Aug 2026
Duties & Responsibilities
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
- Kufanya usafi wa gari;
- Na kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
Qualifications
Kuajiriwa wahitimu wenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
